Thursday, April 12, 2018

TASAF kuwezesha umwagiliaji Pemba
WALENGWA 175 waliomo kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini unaoendeshwa na TASF III, Shehia ya Kendwa wilaya ya mkoani Pemba, wanatarajiwa kuwanufaisha wakulima wa mpunga 220 wa bonde la Egeyani, kuwa na kilimo cha uhakika kuanzia msimu ujao.
Walengwa hao kwa sasa wapo kwenye bonde hilo wakichimba mifereji ya kisasa ya umwagiliaji, ili kuliwezesha bonde hilo kuondokana na mfumo wa ziwa, kutokana na maji yaliyokuwepo kwa muda mrefu, kutokuwa na manufaa kwa wakulima.
Mwandishi wa habari hizi, ameshushuhudia kazi ya kuchimba mifereji kwenye bonde hilo iikiendelea kwa kasi, ambapo miundombinu inayowekwa kwenye bonde hilo, sasa itakinga uwepo wa maji ya bahari.
Naye Msimamizi Mkuu wa wanakaya waliomo kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini katika Shehia hiyo, Salim Mbarouk Salim alisema lengo ni kuona maji ya mvua na yale ya chumvi yanakuwa na njia moja.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima wa bonde hilo wamesema, mpango huo ulioibuliwa na walengwa hao, unafaa kuenziwa na kulindwa kwakuwa matunda yake ni ya kudumu.
Aidha, Mratibu wa TASAF Pemba Mussa Said Kisenge amesema malengo hasa ya miradi ya aina hiyo inayoibuliwa na walengwa, ni kuwa na maendeleo endelevu.
Mradi huo huo unafadhiliwa na TASAF, unalenga kuwapatia uhakika wa kilimo wakulima na ni wa kisasa kuliko miradi yote kisiwani Pemba.
Uchimbaji wa mirefeji ya umwagiliaji ya kisasa Mkoa wa Kusini Pemba chini ya udhamini wa TASAF
      

Monday, April 9, 2018

Kutoka Masasi



Ubovu wa barabara katika Halmashauri ya mji wa Masasi na kijiji cha Mkarango ambacho kimo ndani ya halmashauri ya mji. Mpiga picha ameshuhudia hali hii hivi leo hii inahatarisha maisha ya wakazi wa maeneo kwa kiwango kikubwa sana.

Meeting


Tukiwa katika ofisi zetu za TADIO at ODL TOWER, Open University Dar Es Salaam