Thursday, March 29, 2018

ZIARA FUPI ILOFANYIKA VISIWANI ZANZIBAR


Kufuatia maelekezo ya Bodi ya kusajiliwa  kwa TADIO huko Tanzania Visiwani, viongozi wa TADIO( P. Kwigize -M/kiti, Marco Mipawa- Katibu na Ali Khamis-mjumbe Machi 24'2018 wamefanya zoezi hilo kwa mafanikio makubwa. Zoezi hilo Limefanyikia ktk Ofisi ya Mlajisi wa Mali, Biashara na Makampuni, wizara ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

Viongozi hao wakuu wameweza kuelezea kwa ufasaha maana, nia na malengo makuu ya TADIO ambapo serikali ya Zanzibar imeelewa na kukubali kuisajili TADIO bila shaka yoyote.

Pamoja na shughuli hiyo, viongozi pia wamefanikiwa kutembelea baadhi ya vituo vya Radio wanachama wa TADIO vilivyuko mjini Unguja ambavyo ni
ADHANA FM na Zenj FM na kukutana na viongozi kwa nia ya kufahamiana.